Na Athman Hamza, Gerezani
IMEELEZWA kwamba vibaka wanaoibia abiria kwenye daladala hasa wanawake kwa kuwachania mikoba yao, wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi.
Kwa mujibu wa wataalamu wa fya, endapo kifaa anachotumia kibaka huyo kuchana mkoba wa mwanamke au mfuko wa suruali wa mwanaume na ukapenya hadi kwenye ngozi, ni hatari kubwa ya kuambukiza Ukimwi.
Akizungumza na gazeti hili, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba, alisema aliekatwa atakuwa katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi kama wembe huo utakuwa umemkata mtu mwenye Ukimwi ndani ya dakika mbili, kwani virusi vya Ukimwi haviwezi kukaa katika hewa kwa zaidi ya dakika mbili.
Alisema haifahamiki vibaka hao vifaa wanavyotumia walichukuwa muda gani kumkata abiria mmoja na kwenda kumkata mwingine.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo, endapo kibaka huyo alitumia muda mfupi katika kumkata abiria mmoja na muda huo huo kumkata abiria mwingine na mmoja kati ya abiria hao akawa ana maambukizi ya virusi, moja kwa moja watakuwa wamesababisha maambukizi ya virusi kwa abiria ambaye hakuwa navyo.
Ufafanuzi huo umekuja baada ya abiria mmoja mwanamke kuchanikwa mkoba wake na kuibiwa fedha zake zote.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyekuwa kwenye kituo cha daladala cha Gongo la Mboto kilichopo Kariakoo karibu na kituo cha polisi cha Gerezani, Maria Silvatory mkazi wa Airport, alisema hana uhakika kama nyembe hizo zinakuwa salama, kwani si rahisi kwa wezi hao kununua viwembe vipya na maalumu kwa kazi hiyo tu, kwani kama nao pia wanatumia nyembe hizo katika matumizi yao au kuwakata watu tofauti.
Naye Ofisa Mtendaji wa kata ya Gerezani Felix Nyange, alipotakiwa kuelezea njia anazotumia katika kukomesha tabia ya vibaka hao, alisema kuwa kwa sasa wamekuwa na ushirikiano na jeshi la polisi ambapo majira ya kuanzia saa 11 jioni, Sungusungu wa kata hiyo wamekuwa wakishirikiana na polisi jamii kufanya msako wa vibaka na wezi, hali ambayo imeongeza usalama wa watu na mali zao.
Alisema atawaomba askari jamii hao kwa kushirikiana na mgambo wa kata kuweka ulinzi katika kituo cha Mbagala na Gongo la Mboto hususani nyakati za jioni ambapo abiria wanagombania mabasi.
"Tutaanza kuweka mgambo na polisi jamii katika vituo hivyo ili kupunguza kero hiyo ambayo abiria wamekuwa wakikabiliana nayo kila siku," alisema Nyange.
Msomaji wetu kwanza tunakupongeza kwa kutumia hii blog hii kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea jijini hususani zinazohusu Dala dala. Lengo la Blog hii ni kuishurutisha jamii ya watanzania ili kushinikiza maendeleo. Kwa kutumia Dala Dar Leo, usafiri Dar es salaam utabadilika na kuwa na mazingira mazuri kiasi cha kuruhusu watu wengi zaidi kuutumia. Hivyo tunaamni hili litakuwa ni jukwaa lako la kushiriki katika mijadala mbalimbali ili kuboresha huduma hiyo muhimu. Asante Mhariri
DarLeo
Usikubali kupitwa na Darleo kila siku jioni kwa Habari na matukio ya leo leo. Gazeti pekee la kila siku jioni. Sasa limesheheni habari moto moto kutoka mtaani kwako.
Wednesday, February 9, 2011
Subscribe to:
Comments (Atom)